Pata taarifa kuu
TANZANIA-JOHN MAGUFULI-SHULE-VIBOKO

Magufuli aunga mkono adhabu ya viboko kwa wanafunzi

Adhabu ya viboko kwa wanafunzi ni marufuku kisheria kwa mujibu wa sheria za Tanzania
Adhabu ya viboko kwa wanafunzi ni marufuku kisheria kwa mujibu wa sheria za Tanzania RFI/RM

Rais wa tanzania ameunga mkono adhabu kwa wanafunzi wa shule nchini Tanzania, siku moja baada ya kusambaa taarifa mtandaoni zikimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert chalamila akiadhibu kwa viboko wanafunzi wa shule moja ya sekondari nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Chalamila alikuwa akizuru shule ya sekondari ya Kiwanja iliyopo wilayani Chunya, Kusini magharibi mwa Tanzania.

Akiwa ziarani Mkoani Songwe, Rais Magufuli ametoa pongeza kwa mkuu huyo wa mkoa wa Mbeya.

''Leo nilikuwa naongea na mkuu wa mkoa wa Mbeya nikamwambia nakupongeza sana kwa kuwatandika wale viboko na nikawaambia uliwatandika viboko vichachee...haiwezekani serikali tunatoa mabilioni kwa ajili ya kujenga madarasa na shule halafu mtoto anaenda kuichoma''. Alisema rais Magufuli.

Aidha kiongozi huyo mkuu wa Tanzania ameagiza kufukuzwa shule kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita waliochoma moto majengo ya shule hiyo sanjari na kuvunjwa kwa bodi ya shule hiyo ya s erikali.

Rais huyo ambae yupo ziarani katika eneo la nyanda za juu kusini amesema kuwa alimwambia Bwana Chalamila awafukuze watoto wote waliohusika na tukio hilo .

''Nikamwambia watoto hao wote fukuza wote, kwa hiyo watoto wote wamefukuzwa, na bodi imevunjwa kwasababu ile pia uzembe wa bodi ya shule hiyo..eti haki za binadamu, haki za binadamu watoto wawe na viburi vya kipumbavu hivyo. Ni lazima tuache mchezo katika maendeleo'', alisema.

Ameonya kuwa kurudi shuleni kwa watoto hao ni lazima baba zao walipie gharama za majengo yaliyoharibiwa na akaagiza kuwa wale ambao walihusika wapelekwe jela.

Adhabu ya viboko kwa wanafunzi wa shule nchini Tanzania haizuiwi kwa mujibu wa sheria za taifa hilo la Afrika mashariki.

 

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.