RWANDA-MAREKANI-USALAMA

Rwanda yamfukuza mhubiri wa Kiinjili kutoka Marekani

Serikali ya Rwanda imeamua kumfukuza mhubiriwa wa Kiinjili kutoka Marekani, Gregg Schoof.
Serikali ya Rwanda imeamua kumfukuza mhubiriwa wa Kiinjili kutoka Marekani, Gregg Schoof. Getty/Peter Stuckings

Rwanda imesema Mhubiri na mmiliki wa kituo cha redio cha Amazing Grace, Gregg Schoof, raia wa Marekani aliyekamatwa mapema wiki hii jijini Kigali, amefukuzwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Schoof amekuwa nchini Rwanda tangu mwaka 2003, kuhubiri lakini mwaka uliopita, kituo chake che redio kilifungwa baada ya kuhubiri kupitia redio yake kuwa, wanawake ni malaya na ibilisi.

Alikamatwa siku ya Jumatatu, akiwa na mwanaye wakati alipokuwa anataka kuwahotubia wanahabari jijini Kigali akilenga kuishtumu seirkali ya Rwanda.

Idara ya uhamiaji inasema, mtoto wake ambaye hakutajwa jina aliachiliwa huru lakini, baba yake amefukuzwa kwa sababu mbili, kwanza, kibali chake cha kufanya kazi kilikuwa kimeisha lakini pia hakuwa na sababu ya kuwa Rwanda kwa sababu kituo chake cha redio kilishafungwa.

Kanisa la Mhubiri huyo ni miongoni mwa Makanisa 700 yaliyofungwa mwezi Februari, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya serikali kuhusu kufungua kanisa.