Pata taarifa kuu
KENYA-Al SHABAB-USALAMA

Polisi ya Kenya yaimarisha usalama Kaunti ya Mandera

Kikosi cha Ulinzi cha Kenya baada ya shambulio la wanamgambo wa Al Shabab katika Chuo Kikuu cha Garissa Aprili 2015.
Kikosi cha Ulinzi cha Kenya baada ya shambulio la wanamgambo wa Al Shabab katika Chuo Kikuu cha Garissa Aprili 2015. CARL DE SOUZA / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Polisi katika Kaunti ya Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya wapo katika hali ya tahadhari, baada ya kuripotiwa kuwa washukiwa 20 wa Al Shabab kutoka nchini Somalia walikuwa wameonekana katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, magaidi hao walionekana katika maeneo ya Bale-Ilman Mala na Kutulo Ijumaa iliyopita.

Haya yanajiri wakati huu miili ya maafisa 11 wa polisi waliouawa Jumamosi iliyopita huko Garissa wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi kilichotegwa ardhini ikirejeshwa jijini Nairobi.

Kenya imeendelea kuwa kwenye vita na kundi la Al Shabab tangu mwaka 2011, ilipotuma wanajeshi wake nchini humo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.