SUDANI-SIASA-SIASA-USALAMA

Wasiwasi waendelea kutanda Sudani Kusini kabla ya Novemba 12

Kiongozi wa waasi wa Sudani Kusini Riek Machar wakati wa kutia saini kwenye mkataba wa amani na serikali ya Sudani Kusini.
Kiongozi wa waasi wa Sudani Kusini Riek Machar wakati wa kutia saini kwenye mkataba wa amani na serikali ya Sudani Kusini. © REUTERS

Raia wa Sudani Kusini wanaendelea kuingiliwa na wasiwasi, huku baadhi yao wakisema tarehe 12 Novemba 2019 inawatia wasiwasi. Tarehe 12 Novemba 2019, ni siku ambayo kiongozi wa waasi Riek Machar anatarajiwa kurudi Juba na kuunda serikali ya umoja na Rais Salva Kiir.

Matangazo ya kibiashara

Tayari Riek Machar amesongeza mbele mara kadhaa tarehe ya kurudi kwake nchini Sudani Kusini. Kiongozi wa waasi alitarajiwa kurudi Juba mwezi Mei, lakini tzoezi hilo lilisogezwa mbele kwa miezi sita, na upinzani unaomba tarehe ya mwisho kwani kuchelewesha kwa utekelezaji wa mkataba wa amani uliotiliwa saini 2018 ni muhimu. Katika siku za hivi karibuni, wasiwasi umeendelea kuongezeka kadri siku zinavyokwenda.

Kwa mara nyingine tena, Kanisa Katoliki la Sudani Kusini linasema "lina wasiwasi" siku hiyo ya tarehe 12 Novemba inapokaribia. Kanisa Katoliki linawakumbusha wahusika "jukumu lao la kuendeleza nchi mbele bila vurugu".

Hivi karibuni Rais Salva Kiir alitangaza kwamba ikiwa Riek Machar atakuwa hajarudi kwa tarehe iliyopangwa, ataamua kuunda serikali mwenyewe. Hali ambayo inaweeza kuzusha tena mapigano katika taifa hilo changa barani Afrika, wakati vikosi kutoka pande zote vimeanza kujipanga kwa kujiandalia vita.

Askofu Mkuu Justin Badi Arama anasisitiza kwamba serikali yoyote itakayoundwa iwe ya umoja. Lakini "ikiwa tofauti zilizopo zitakuwa bado hazijatatuliwa kabla ya tarehe 12 Novemba 2019, ni bora zaidi zoezi la kuunda serikali mpya lisitishwe," amesema.

Kiongozi wa waasi Riek Machar ameomba tarehe ya mwisho ya miezi sita. Kwa upande wa kambi yake, zoezi la kuunda jeshi la kitaifa limechelewa sana. Msemaji wake Mabior Garang Mabior amesema "sekta nzima ya usalama inatakiwa kurekebishwa, ili kuwepo na amani na kila mtu aweze kurejea nyumbani", amesema Bw Garang Mabior. Sio swali la kuunda kikosi tuu cha walinzi wa taasisi ", ameongeza.

Jumatatu wiki hii, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uholanzi, Sweden, Uswisi na Uingereza wametia saini taarifa ya pamoja kuelezea kwamba "mengi bado yanapaswa kufanywa hadi tarehe 12 Novemba".