RWANDA-UGANDA-UCHUMI

Mvutano kati ya Rwanda na Uganda wazorotesha shughuli mbalimbali mpakani

Wilaya ya Musanze nchini Rwanda
Wilaya ya Musanze nchini Rwanda Thomas Mukoya/Reuters

Eneo la Kaskazini mwa Rwanda, raia wanaoishi karibu na mpaka na nchi ya Uganda wamesema wameathirika pakubwa na mvutano baina ya nchi hizo mbili ambazo kila mmoja anamtuhumu mwenzake kwa kusababisha usalama duni.

Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wa RFI idhaa ya Kifaransa Lor-Brular, anasema licha ya mwezi Agosti mwaka huu rais Paul Kagame na mwenzake Yoweri Museveni kutiliana saini makubaliano ya kumaliza tofauti zao, shughuli nyingi za kibiashara katika mji wa Musanze zimeendelea kuzorota huku raia wakilalamikia bidhaa kupanda bei.

Katika mji wa Musanze ambao ni wapili kwa ukubwa nchini Rwanda, mwandishi wetu amekutana na baadhi ya wachuuzi wa matunda ambao wamethibitisha kuwa katika wakati mgumu.

Hali inayowakuta wachuuzi wa dogo ndio hali inayoshuhudiwa pia katika maduka ya bidhaa nyingine kama mchele ambao unaelezwa kupanda bei maradufu.