SUDANI KUSINI-MACHAR-SIASA-USALAMA

Mvutano kati ya Salva Kiir na Riek Machar wazua wasiwasi Sudani Kusini

Kiongozi wa waasi Riek Machar aliwasili nchini Sudani Kusini ambapo alikutana kwa mara ya pili tangu Septemba na Rais Salva Kiir kuandaa kurudi kwake kwa mara ya mwisho tarehe 12 Novemba.
Kiongozi wa waasi Riek Machar aliwasili nchini Sudani Kusini ambapo alikutana kwa mara ya pili tangu Septemba na Rais Salva Kiir kuandaa kurudi kwake kwa mara ya mwisho tarehe 12 Novemba. ALEX MCBRIDE / AFP

Tofauti kubwa kati ya mahasimu wawili wa Sudan Kusini, rais Salva Kiir na kiongozi mkuu wa upinzani Riek Machar, inatishia kuitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mwingine, wakati huu muda wa mwisho kwa viongozi hao kuunda Serikali ya umoja wa Kitaifa ambao ni  tarehe 12 mwezi ukikaribia.

Matangazo ya kibiashara

Mvutano uliopo, ikiwa hautatafutiwa suluhu ndani ya takribani wiki
moja iliyosalia, huenda ukaitumbukiza Sudan Kusini katika mgogoro
mkubwa wa kikatiba na hata kurejelewa kwa mapigano baina ya pande hizo
mbili.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na mataifa kadhaa ya
magharibi, wanazitaka pande hizo mbili kuhakikisha wanaunda Serikali
ndani ya muda uliopangwa.

Raia wa Sudani Kusini wana wasiwasi ya kuzuka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha vifo na umati wa watu kurudi kuyahama makaazi yao kama ilivyotokea katika miaka ya hivi karibuni.

Tayari Riek Machar amesogeza mbele mara kadhaa tarehe ya kurudi kwake nchini Sudani Kusini. Kiongozi wa waasi alitarajiwa kurudi Juba mwezi Mei, lakini tzoezi hilo lilisogezwa mbele kwa miezi sita, na upinzani unaomba tarehe ya mwisho kwani kuchelewesha kwa utekelezaji wa mkataba wa amani uliotiliwa saini 2018 ni muhimu. Katika siku za hivi karibuni, wasiwasi umeendelea kuongezeka kadri siku zinavyokwenda.

Kiongozi wa waasi Riek Machar ameomba tarehe ya mwisho ya miezi sita. Kwa upande wa kambi yaMachar wanasema, zoezi la kuunda jeshi la kitaifa limechelewa sana. Msemaji wake Mabior Garang Mabior amesema "sekta nzima ya usalama inatakiwa kurekebishwa, ili kuwepo na amani na kila mtu aweze kurejea nyumbani", amesema Bw Garang Mabior. Sio swali la kuunda kikosi tuu cha walinzi wa taasisi ", ameongeza.

Hivi karibuni Rais Salva Kiir alitangaza kwamba ikiwa Riek Machar atakuwa hajarudi kwa tarehe iliyopangwa, ataamua kuunda serikali mwenyewe. Hali ambayo inaweeza kuzusha tena mapigano katika taifa hilo changa barani Afrika, wakati vikosi kutoka pande zote vimeanza kujipanga kwa kujiandalia vita.