SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA
Hali ya wasiwasi yaendelea kutanda Sudani Kusini
Mazungumzo kati ya pande zinazohasimiana nchini Sudan Kusini yameahirishwa kwa siku mbili, wakati huu kukiwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuundwa kwa Serikali ya umoja ifikapo Novemba 12.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Mazungumzo kati ya rais Salva Kiir na mwenzake Riek Machar yalikuwa yafanyike Jumanne wiki hii lakini yakaahirishwa bila ya uwepo wa sababu za msingi.
Taarifa kutoka taasisi zinazosimamia mchakato wa amani nchini humo, zinasema kuwa viongozi hao wawili hawajaonesha nia ya kuwa tayari kufanya kazi pamoja.
Aidha madai ya rais Kiir kuwa ataunda Serikali peke yake bila ya Machar yanazidisha sintofahamu zaidi kuhusu mustakabali wa nchi hiyo.