URUSI-BURUNDI-USHIRIKIANO

Urusi yaunga mkono Burundi na kukanusha dhulma dhidi ya upinzani

Sergei Lavrov : "Tumesema kwamba Mataifa ya kigeni kuingilia masuala ya ndani ya Burundi haikubaliki".
Sergei Lavrov : "Tumesema kwamba Mataifa ya kigeni kuingilia masuala ya ndani ya Burundi haikubaliki". © Mladen ANTONOV / AFP

Urusi imethibisha uungwaji wake mkono kwa taasisi za nchi ya Burundi ikiwa imesalia miezi michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Burundi ambayo inakosolewa na jumuiya ya kimataifa, kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ukandamizaji dhidi ya upinzani, kwa sasa inaweza kutegemea msaada kutoka Urusi ... Kama ilivyothibitishwa wakati wa mapokezi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ezekiel Nibigira na mwenyeji wake Sergei Lavrov jijini Moscow Jumanne wiki hii.

Hakuna maswala ya kuilaumu Burundi kwa vurugu zilizotokea nchini, kufuatia mzozo wa mwaka 2015 - hakuna maswala ya kukosoa viongozi wa serikali ya Bujumbura, kwa ukandamizaji dhidi ya upinzani, Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov - alibaini jana Jumanne baada ya mazungumzo na mwenzake wa Burundi.

"Tumethibitisha msimamo wetu usiobadilika kuhusu uhuru wa Burundi. Na tukasema kwamba kuingiliwa kwa mataifa ya kigeni katika maswala ya ndani ya Burundi haikubaliki. "

Urusi tayari imeonyesha uungwaji wake mkono kamili kwa viongozi wa Burundi, tofauti na nchi za Magharibi. Huu ni ujumbe ambao viongozi wa Serikali ya Bujumbura wanapongeza. Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ezekiel Nibigira, amekumbusha msaada wa Urusi kwa Burundi.

"Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali na wananchi wa wa Urusi ... Hapa ningependa kusisitiza misaada mbalimbalii Burundi inayopata kutoka Urusi ... Misaada mbalimbali muhimu ya Urusi kwa burundi inaonyesha uhusiano wa ndani kabisa kati ya nchi hizi mbili. "

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya nje wa Burundi ametoa wito kwa wawekezaji wa Urusi kuja kuwekza nchini Burundi:.

"Njooni mjionee wenyewe kuwa kila kitu kinaenda vizuri katika nchi yetu," amesema Bw Nibigira, kabla ya kubaini kwamba Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 utakuwa uchaguzi wa kuaminika kidemokrasia na wa wazi".