Pata taarifa kuu
KENYA-MAENDELEO

Mkutano kuhusu masuala ya idadi ya watu na maendeleo kuanza Jumanne Nairobi

Mji mkuu wa Kenya Nairobi. Kenya itakuwa mwenyeji ya mkutano kuhusu masuala ya idadi ya watu na maendeleo.
Mji mkuu wa Kenya Nairobi. Kenya itakuwa mwenyeji ya mkutano kuhusu masuala ya idadi ya watu na maendeleo. Photo by Thomas Imo/Photothek via Getty Images
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Maelfu ya wajumbe kutoka mataifa mbalimbali duniani wapo jijini Nairobi nchini Kenya, kuhudhuria mkutano wa siku tatu, unaoanza Jumanne wiki hii kujadili masuala ya idadi ya watu na maendeleo.

Matangazo ya kibiashara

Idadi kubwa ya wajumbe hao ni vijana, lakini pia mkutano huo unatarajiwa kugusia masuala yanayowaathiri vijana hasa afya, mapenzi na suala la upangaji uzazi.

Viongozi wa Kanisa Katoliki wameshtumu hatua ya Kenya kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo na kusema kuwa Kanisa hilo halitahudhuria mkutano huo.

Rais wa muungano wa mashirika ya kiraia nchini Kenya Suba Churchil, amesema baadhi ya watu hawajaelewa kiini cha mkutano huo.

Wadadisi wanasema idadi ya watu barani Afrika inakuwa kwa kasi ambapo kufikia mwaka 2050 itakuwa imeongezeka maradufu ya ilivyo sasa, huku 40% ya watu masikini kabisa duniani wakihofiwa kuja kuishi kwenye mataifa mawili tu ya bara hilo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.