TANZANIA-KENYA-UGANDA

FAO;Wakulima wahimizwa kujikita kwenye kilimo hai ili kuongeza tija ya Mazao

Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini Tanzania ,Fred Cafeerom Balozi wa Ufaransa nchini humo Frederic Clavier na Cecil Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Utamaduni kutoka Ubalozi wa Ufaransa.
Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini Tanzania ,Fred Cafeerom Balozi wa Ufaransa nchini humo Frederic Clavier na Cecil Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Utamaduni kutoka Ubalozi wa Ufaransa. Picha:FAO

Shirika la Chakula Duniani FAO limesema kilimo cha kutumia Mbolea za kemikali kimechangia kwa asilimia kubwa kuongezeka kwa ukosefu wa chakula katika nchi zinazoendelea hali inayolazimu wakulima kuanza kujifunza kilimo hai ili kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza hii leo jijini Dar es salaam, Mwakilishi mkazi wa FAO nchini Tanzania Fred Cafero amesema kilimo hai ni kinaongeza tija kwa Mkulima

Cafero ameongeza kuwa Kilimo hai kimesaidia kuimarisha Usalama na Uhakika wa Chakula pamoja na Kuhimili mabadiliko ya tabianchi na uhifadhi wa mazingira.

Nchini Tanzania,Ubalozi wa Ufaransa umewasaidia wakulima wadogo 6,000 katika mradi wa utunzaji wa ekolojia na kuhifadhi mazingira mkoani Mtwara nchini Tanzania, Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Utamaduni kutoka ubalozi wa Ufaransa nchini humo amesema ubalozi umewawezesha Fedha wakulima hao zaidi ya Dola za kimarekani Milioni moja.

Frederic Clavier Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania anasema kilimo cha kemikali kinaathari kwa Dunia.

    "Mfumo wa kilimo cha kemikali kimesababisha upotevu wa miti,ukosefu wa maji, upotevu wa Viumbe Hai, uharibifu wa ardhi na uzalishaji wa hewa ya ukaa, na hii ni Dunia nzima"-alisema Balozi Clavier.

Kwa Upande wake Mshauri wa Mawasiliano kutoka Shirika la kuendeleza kilimo hai Tanzania Constantine Akitanda amesema kilimo hicho kimewasaidia wakulima kupata mazao mengi yenye faida kubwa katika soko,kuhifadhi mazingira pamoja na maji yanayopatikana ardhini huku Ekokolojia iliyopo ardhini ikiendelea kuhifadhiwa.

Novemba 27 na 28 mwaka huu utafanyika Mkutano wa Kitaifa nchini humo kuangazia namna ya kuongeza matumizi ya mifumo ya ikolojia katika kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa za kilimo kwa usalama wa chakula, kutokomeza umaskini, kuongeza uchumi na kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ili kuwa na kilimo endelevu.