RWANDA-PAUL KAGAME-RDF

Kagame:RDF itaendelea kulinda usalama na amani ya Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda akikagua gwaride kabla ya kutunuku nishati kwa maofisa wapya wa kijeshi
Rais Paul Kagame wa Rwanda akikagua gwaride kabla ya kutunuku nishati kwa maofisa wapya wa kijeshi www.newtimes.co.rw

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema Jeshi la nchi hiyo litaendelea kutimiza wajibu wake muhimu wa kulinda amani, mipaka na usalama wa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kagame ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Rwanda ametoa matamshi hayo wakati wa hafla ya kutunuku maafisa zaidi ya 320 waliohitimu mafunzo mbalimbali ya kijeshi katika kambi ya Bugesera nchini humo.

Kiongozi huyo pia ametoa pongezi kwa maofisa waliochagua taaluma za kijeshi kuitumikia nchi ya Rwanda huku pia akionyesha furaha yake kwa namna jeshi hili lilivyo na ushirikiano na wananchi.

RDF iliundwa baada ya kumalizika kwa mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994.