TANZANIA-JOHN POMBE MAGUFULI-CCM-CHADEMA-CUF-DEMOKRASIA

Kipyenga cha kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa chapulizwa Tanzania, upinzani ukiweka msimamo wa kutoshiri uchaguzi

Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema. Chama hicho ni miongoni mwa vyama saba vilivyosusa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa
Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema. Chama hicho ni miongoni mwa vyama saba vilivyosusa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa BBC

Filimbi ya kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa imepulizwa ambapo kampeni za uchaguzi huo zinaanza hii leo. 

Matangazo ya kibiashara

Kampeni hizo zinaanza leo na zinatarajiwa kukamilika siku moja kabla ya uchaguzi ambao utafanyika Novemba 24 katika eneo lote la Tanzania Bara.

Hata hivyo uchaguzi huo unafanyika wakati vyama saba vya upinzani vikiwa vimetangaza kususia uchaguzi huo huku kwa madai ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi, vikitoa wito kwa rais wa taifa hilo, John Magufuli kufuta uchaguzi huo.

Vyama vilivyosusa kushiriki uchaguzi huo ni CUF, Chadema, ACT Wazalendo, Chaumma, NLD,UPDP,CCK na NCCR Mageuzi.

Chama lawala cha CCM kupitia katibu wake wa itikadi na uenezi Humphrey Polepole kimesema kitashiriki uchaguzi huo na kuahidi kufanya kampeni za kistaarabu huku kikishutumu vyama vya upinzani kwa kuwa na ajenda ya kususia uchaguzi.

Viongozi wa kitaifa akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wameonya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayeleta fujo katika uchaguzi huo.

Hata hivyo vyama vingine vya upinzani kikiwemo TLP vimesema vitashiriki uchaguzi huo.

Kujiondoa kwa vyama vya upinzani kumezua mjadala mpana miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii huku baadhi yakiunga mkono na mengine yakipinga hatua hiyo.

Uchaguzi waserikali za mitaa nvchini Tanzania hufanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu.