Pata taarifa kuu
KENYA-MAFURIKO-MVUA-MSAADA

Watu 29 wapoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo nchini Kenya

Maporomoko ya udongo katika Kaunti ya Pokot Magharibi nchini Kenya Novemba 23 2019
Maporomoko ya udongo katika Kaunti ya Pokot Magharibi nchini Kenya Novemba 23 2019 Kenya Red Cross
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Watu 29 wamepoteza maisha katika Kaunti ya Pokot Magharibi nchini Kenya, baada ya kutokea kwa maporomoko ya udongo kutokana na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko makubwa katika eneo hilo. 

Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi wa serikali katika Kaunti hiyo Apollo Okello amesema, miongoni mwa watu waliopoteza maisha, ni wanawake na watoto, na jitihada zinaendelea kuwatafuta watu wengine ambao hawajapatikana.

Hata hivyo, juhudi hizo zinanatizwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha ambayo imeharibu miundo mbinu ya mawasiliano kama barabara.

Rais Uhuru Kenyatta amesema, serikali yake inafanya kila inachowezesha kuwasaidia waathiriwa wa janga hilo na ameagiza polisi kutumia ndege aina ya helikopta kurahihisha uokozi huo.

"Tunajitahidi sana kuwasaidia watu waliothirika na kuwatafuta wale ambao hawajapatikana," amesema Eugene Wamalwa, Waziri wa serikali.

Aidha, imebainika kuwa, maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni vijiji vya Nyarkulian na Parua ambavyo vilishuhudia mvua kubwa kuanzia siku ya Ijumaa.

Kwa sasa, barabara kutoka miji ya Kitali na Lodwar, haipitiki huku daraja linalotegemewa la Muruny, likisombwa na maji huku maafisa wa uokoaji na hata wale maafisa wa msalaba mwekundu wakishindwa kufikisha misaada kama chakula na dawa.

Wakaazi wa Kaunti hiyo, wanasema hawajawahi kushuhudia janga kama hili.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.