Pata taarifa kuu
TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA

Marekani na Uingereza zatilia shaka uhalali wa uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania

Baadhi ya wanawake wa Kitanzania wakipiga kura zanzibar
Baadhi ya wanawake wa Kitanzania wakipiga kura zanzibar TONY KARUMBA / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Marekani na Uingereza kupitia mabalozi wao nchini Tanzania zimehoji uhalali wa uchaguzi wa serikali mita na matokeo yake, uchaguzi uliofanyika Jumapili, Novemba 24 mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Mabalozi wa Marekani na Uingereza wamesema hawakuridhishwa na jinsi uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyoesimamiwa na kuendeshwa nchini Tanzania.

Katika taarifa zao balozi hizo mbili zimelaani msimamo wa wasimamizi wa uchaguzi huo wa kuwatenga wagombea kutoka vyama vya upinzani katika mchakato wa uchaguzi.

'Marekani inasikitishwa na taarifa za ukiukwaji katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa'', taarifa ya balozi ya Marekani imesema.

“Hali hii ya mkanganganyiko inazua swali kuhusu uhalali wa mchakato wa uchaguzi na matokeo”, imesem ataarifa ya balozi ya Uingereza.

Jumla ya vyama vikuu vinane vilijitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa umesalia mwaka mmoja kabla ya nchi hiyo kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu.

Vyama vilivyotangaza kujitoa kushiriki kinyang'nyiro cha uchaguzi huo ni Chadema, UMD, CCK, NCCR-Mageuzi, NLD, ACT-Wazalendo, CUF na Chauma.

Uamuzi wao ulitokana na malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa mbele ya umma na kukilaumu chama tawala CCM Uamuzi wao ulitokana na malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa mbele ya umma na kukilaumu chama tawala CCM kuwa chanzo cha kuvurugika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu nchini.

Upinzani unadai kuwa mchakato mzima wa uchaguzi huo ulitawaliwa na udanganyifu uliotekelezwa na Chama tawala CCMkwa ushirikiano na maafisa wa uchaguzi.

Katika baadhi ya maeneo wagombea wa CCM walipita bila kupingwa.

Kwa upande wake, Chama tawala nchini Tanzania CCM kimesema kilishinda kwa zaidi ya asilimia tisini katika uchaguzi huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.