RWANDA-UKIMWI-AFYA

Rwanda na nchi kadhaa kujadili namna ya kudhibiti maambukizi ya UKIMWI Afrika

Serikali ya Rwanda inaendelea kuhimiza wananchi wake namna ya kupambana dhidi ya maambukizi ya virisi vya UKIMWI.
Serikali ya Rwanda inaendelea kuhimiza wananchi wake namna ya kupambana dhidi ya maambukizi ya virisi vya UKIMWI. TONY KARUMBA / AFP

Kongamano la Kimataifa kuhusu maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi, linaanza leo jijini Kigali nchini Rwanda, kujadili namna ya kudhibiti maambukizi hasa kwa vijana barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Hili hili ni kongamabo la pili, baada ya lingine kufanyika jijini Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati dunia ikiadhimisha siku ya kupambamna na maambukizi ya ukimwi hapo jana.

Mwezi Julai mwaka huu Umoja wa Mataifa uliripoti kwamba vifo vinavyotokana na maradhi ya UKIMWI vimepungua kwa asilimia 33 tangu mwaka 2010 lakini fedha zaidi zinahitajika ili kuzuia kuenea kwa maradhi hayo.

Katika ripoti yake ya kila mwaka, Umoja wa Mataifa ulisema vifo vinavyosababishwa na maradhi ya UKIMWI vilipungua kwa takriban vifo 770,000. Idadi hiyo inawakilisha asilimia 33 ya vifo vilivyotokea mnamo mwaka 2010 ambapo watu milioni 1.2 walikufa. Hata hivyo katika ripoti yake Umoja wa Mataifa ulisema maambukizi yameongezeka katika Mashariki ya Kati na Ulaya Mashariki.

Umoja wa Mataifa umeitaka jumuiya ya kimataifa iweke mkazo katika juhudi za kuyakabili maradhi hayo. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo watu wapatao milioni 37.9 wanaishi na virusi vya UKIMWI  duniani. Watu milioni 23.3 wenye virusi hivyo wanapata dawa za kudhibiti maambukizi. Hata hivyo bado pana hali ya wasiwasi.

Umoja wa Mataifa ulisema licha ya hatua hiyo ya mafanikio iliyopigwa, juhudi za kuutokomeza ugonjwa huo zimelegalega kutokana na ufadhili wa fedha wa kiwango cha chini na pia kutokana na watu walio katika baadhi ya maeneo kutopata huduma muhimu za afya.

Katika ripoti yake Umoja wa Mataifa ulisema idadi ya vifo imepungua kwa kiwango kikubwa katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, ingawa mikasa ya maambukizi bado ni mingi. Hata hivyo vifo kutokana na UKIMWI vimeongezeka kwa asilimia 5 katika nchi za Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini na Ulaya Mashariki.