Pata taarifa kuu
UFARANSA-ELIMU-TANZANIA

Ufaransa yanuia kuongeza idadi ya wanafunzi wa kigeni wanaopata ufadhili wa masomo kufikia laki tano

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier akizungumza na waandishi wa habari jana Desemba 3 mwaka 2019
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier akizungumza na waandishi wa habari jana Desemba 3 mwaka 2019 RFI/Fredrick Nwaka
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Nchi ya ufaransa imeweka lengo la kuongez aidadi ya wanafunzi wa kigeni wanaopata ufadhili wa masomo kutoka laki tatu na ishirikini na nne elfu hadi kufikia laki tano miaka michache ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Mpango huo umewekwa wazi na balozi wa Ufaransa nchini Tanzania ,Frederic Clavier wakati wa kongamano la pamoja lililowakutanisha wanafunzi kutoka Tanzania waliowahi kusoma nchini humo na wanaotarajia kusoma nchini humo.

“Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameweka lengo la miaka michache ijayo kuwa na wanafunzi zaidi ya laki tano wa kigeni. Vyuo vya Ufarnsa vina zaidi ya kozi elfu mbili zinazotolewa kwa kiingereza, ambazo zitakuwa rais kwa wanafunzi wanaotoka nchi kama Tanzania” amesema balozi Clavier katika kongamano lililofanyika katika kituo cha utamaduni cha Ufaransam Alliance Francaise.

Tayari baadhio ya wanafunzi waliosoma nchini Ufaransa wamefungua jukwaa maalumu mtandaoni kwa lengo la kutoa mafunzo na maelekezo kwa watu wanaonuia kupata ufgadhili wa masomo na fursa za ajira.

“Tovuti yetu inafahamika kwa anuani ya www.francealumni.fr. Na tunawakaribisha wote wenye nioa ya kupata maelekezo na ufafanuzi wa namna ya kupata ufadhili wa masomo.

Disemba 14 mwaka huu, kutafanyika kongamano baina ya vyuo vikuu vya Ufaransa na Taznania, kongamano ambapo kwa mujibu wa balozi Clavier litakuwa fursa nyingine kwa watanzani kupata nafasi ya kusoma Ufaransa.

Mwaka 2020, watanzania 30 wamepata ufadhili ambapo wanatarajiwa kwenda kusoma kozi mbalimbali zikiwemo uchumi, uhandishi, maendeleo na kilimo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.