Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-UCHUMI

Spika wa Bunge la Sudani Kusini ajiuzulu

Mji mkuu wa Sudani Kusini Juba.
Mji mkuu wa Sudani Kusini Juba. Aguek/Wikimedia Commons
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Spika wa bunge la Sudani Kusini ametangaza kujiuzulu nafasi yake baada ya wabunge kutishia kumuondoa madarakani wakimtuhumu kuzuia harakati za mapambano dhidi ya rushwa na ubadhilifu.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge wanamtuhumu Anthony Lino Makana kwa kushindwa kuwasilisha bungeni ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali pamoja na kukataa wabunge kuwaitisha mawaziri kujibu maswali.

Nchi ya Sudan Kusini ni miongoni mwa mataifa yanayoorodheshwa kukithiri kwa vitendo vya rushwa hasa kwa maofisa wa juu wa Serikali.

Katika taarifa yake iliyotangazwa na shirioka la habari la Sudan Kusini spika amesema sababu iliyomfanya kujiuzulu ni kuonesha heshima kubwa kwa uongozi wa chama tawala cha SPLM kutokana na chama hicho kumuomba achukua hatua hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.