SUDANI KUSINI-MAREKANI-VIKWAZO

Marekani yatishia kuwanyima viza watu wanaotatiza mchakato wa amani Sudani Kusini

Marekani iliitaka Serikali ya Kenya kuchunguza mali zinazomilikiwa na familia za wasomi kutoka Sudan Kusini, zikiwemo mali za aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na rais Salva Kiir, mali ambazo Marekani inasema viongozi hao wamewekeza nchini Kenya.
Marekani iliitaka Serikali ya Kenya kuchunguza mali zinazomilikiwa na familia za wasomi kutoka Sudan Kusini, zikiwemo mali za aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na rais Salva Kiir, mali ambazo Marekani inasema viongozi hao wamewekeza nchini Kenya. ALEX MCBRIDE / AFP

Marekani imetoa onyo la kuwanyima viza watu wanaoendelea kuwa kikwazo cha kufanikisha juhudi za kupata amani nchini Sudani Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili limetolewa na Waziri wa Mambo ya nje Mike Pompeo, ambaye amesema wananchi wa Sudan Kusini wameteseka vya kutosha kutokana na vita na kucheleweshwa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Hata hivyo, Marekani haijatoa orodha ya watu wanaolengwa lakini imesema watu hao na familia zao watawekewa vikwazo.

Mwezi Juni 2018 Marekani iliitaka Serikali ya Kenya kuchunguza mali zinazomilikiwa na familia za wasomi kutoka Sudan Kusini, zikiwemo mali za aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na rais Salva Kiir, mali ambazo Marekani inasema viongozi hao wamewekeza nchini Kenya.

Marekani ilisema inao ushahidi wa kutosha kuonesha namna familia na viongozi wa Sudan Kusini wamekuwa wakiwekeza nchini Kenya kwa kutumia fedha za uma huku wengi wakiwa kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo.