Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA-MAZINGIRA-ELIMU

Ufaransa Kuongeza Idadi ya Wanafunzi katika Udhamini wa Elimu ya Juu Kutoka Tanzania

Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier akifungua kituo cha taarifa UDSM
Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier akifungua kituo cha taarifa UDSM Picha/Imani Nathanael
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Serikali ya Ufaransa imeongeza Idadi ya wanafunzi watakaopata udhamini wa kwenda kusoma elimu ya juu nchini humo kutoka nchini Tanzania kutoka wanafunzi thelathini hadi kufikia wanafunzi Hamsini.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika Mkutano unaowakutanisha Wanafunzi zaidi ya 900 kutoka katika vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania na wawakilishi wa vyuo 10 vya elimu ya juu nchini Ufaransa jijini Dar es salaam, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier amesema lengo ni kuwapa fursa watanzania kusoma nchini humo.

'Serikali yangu itaongeza udhamini kwa watanzaia hadi sasa tunadhamini wanafunzi thelathini ,tutadhamini hamsini'-alisema Clavier

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania Tate Ole Nasha anasema hiyo ni fursa muhimu kwa wanafunzi wa Tanzania huku akiipigia chepuo lugha ya kiswahili kwa kuvitaka vyo vya elimu ya juu Ufaransa kuanza kufundisha lugha hiyo.

Rais wa Mtandao wa wanafunzi waliosoma nchini Ufaransa Monday Israel kusoma ufaransa kuna tija kwa watanzania kwani hivi sasa vyuo vinavyofundisha kwa kutumia lugha ya kiinereza vimeongezeka.

Wanafunzi wa Elimu ya juu kutoka taasisi ya Teknolojia Dar es salaam DIT Sumaiya Idd Zuberi anasema ni fursa muhimu kwa wanafunzi wanaotoka nchini Tanzania kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kujisomesha.

Mara baada ya Mkutano huo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)nchini Tanzania Profesa Andrea Pembe amesaini mkataba wa makubaliano ya mashirikiano na chuo kikuu cha Boudoux ili kushikiana katika elimu ya Afya na sayansi pamoja na mazingira.

 

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.