KENYA-KRISMASI-SHEREHE-FEDHA

Sherehe za Krismasi yawadia, wakenya walilia hali ngumu ya kiuchumi

Sherehe za Krismasi mwaka 2019
Sherehe za Krismasi mwaka 2019 Wikipedia

Wakiristo kote dunia, wanaadhimisha sikukuu ya Krismasi siku ya Jumatano, siku ambayo wanaamini, mwokozi wao Yesu Kristo alizaliwa, na wengi hutumia siku hii kusherehekea kwa kula na hata kutalii katika maeneo mbalimbali, lakini baadhi ya Wakenya wanasema kipindi hiki ni kigumu kwao kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

Katikati mwa jiji na hata barabara za pembeni zinaskika kelele za magari ,kondakta wakiwaita wateja , mazungumzo ya raia wakibanana  kuelekea maeneo tofauti ya nchi.

Barababa hizi  za jiji la Nairobi na  kuelekea kwenye vituo vikubwa vya mabasi ya kwenda bara Kawaida tarehe kama hizi huwa kumetulia kwa kuwa watu wengi huwa wamekwisha safari kuelekea vijijini au kujiachia likizoni isipokuwa tu wachache .

Hali hata hivyo ni tofauti kutokana na wakenya kukamatika mfuko na gharama ya juu ya usafiri.

 Wachache wanaokaidi hali hii matokeo ni kama haya.

 “Hatujawahi lipa kupita shilingi 2500, kutoka hapa  kuenda upande wowote ya Magharibi (Western  Kenya )  unalipa shilingi 2500 .Watu   wanakimbilia kuingia kwa hayo  magari ,”baadhi ya abiria walisema.

Kwenye soko la chakula la Marikiti mambo pia ni kama hayo .

 “Aii niko  juu ya jiwe,...Mimi najua siendi mashambani. Unaskia  tuko pamoja?Ndo hayo.Hii Krismas haina pesa,”walisema wafanyibiashara soko la Marikiti Nairobi.

Walioko  sekta ya utaliii na hoteli,kilio ni hicho hicho.Hoteli nyingi hazina watu na wachache wanaojimudu wamelazimika kubuni njia mbadala ya  kutogharamika mno.

Hassan Faisal  amekuwa kwenye sekta hii kwa muda na pia meneja mkuu wa hoteli ya Kilua Mombasa.

“Watu wanachukua nyumba zile hazina wenyewe  kwa sasa,wanaanza kuweka watu. Na watu wanapenda sana hilo soko, kwa hiyo hoteli zinapata shida sana kwa sababu nyumba hizo aina za apartments na Villas ndizo zinazochukua kiasi kikubwa cha watu wanaozuru Mombasa. Na hawali kwenye hoteli,wananunua vyakula vyao wanajipikia,”alisikitika Hassan.

Mtalaam wa maswala wa kiuchumi Njumwa Mwikamba  anakiri hali tete na anashauri  hekima kwenye matumizi msimu huu.

“Kama mtu anahitaji kwenda nyumbani kwa ajili ya Krismasi,awe na nauli ya shilingi 3,000 kwenda na elfu tatu zingine kurudi.Yaani uwe na angaa shilingi elfu 30,000 za matumizi ya krismasi tu,”alisema Njumwa.

Tarehe za 25,26 Disemba huwa kisheria zinatambuliwa kuwa siku kuu ulimwengu na Disemba huwa likizo inayoenziwa na wengi.