SUDANI KUSINI-KIIR-MACHAR-SIASA-USALAMA

Sudani Kusini: Washington yaweka shinikizo kwa Salva Kiir na Riek Machar

Kushoto kwenda kulia: Jenerali Mohammed H. Daglo, Hadi Idriss Yahia wa SRF, Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir, na Tut Galwak, wa Kamati ya Upatanishi, Juba, baada ya kutia saini kwenye mkataba wa amani. Oktoba 21, 2019.
Kushoto kwenda kulia: Jenerali Mohammed H. Daglo, Hadi Idriss Yahia wa SRF, Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir, na Tut Galwak, wa Kamati ya Upatanishi, Juba, baada ya kutia saini kwenye mkataba wa amani. Oktoba 21, 2019. REUTERS/Jok Solomun

Rais aw Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa kivita nchini humo, Riek Machar, walikutana siku mbili jijini Juba kujaribu kufufua mazungumzo kwa minajili ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Matangazo ya kibiashara

Awali uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ulikuwa umepangwa kufanyika Mei mwaka jana, lakini uliahirishwa mara mbili. Tarehe mpya na ya mwisho ni mwezi ujao.

Wakati huo huo Marekani imeendelea kuweka shinikizo kwa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa kivita, makamu wake wa zamani Riek Machar, wakati naibu waziri wa mambo ya nje anayehusika na mambo ya Afrika, Tibor Nagy anafanya ziara katika ukanda huo.

Hayo yanajiri wakati Makamu wa rais wa Afrika Kusini David Mabuza, ambaye kwa sasa anaongoza juhudi za usuluhishi wa masuala tata nchini Sudan Kusini kuelekea uundwaji wa seirikali ya pamoja mwezi ujao, amependekeza kuahirishwa kwa upatikanaji wa suluhu kuhusu mzozo wa mipaka na idadi ya majimbo.

Baada ya mazungumzo na rais Salva Kiir, Mabuza amesema imekubaliwa kuwa suluhu ya mzozo huo ipatikane, baada ya siku 90 pindi tu serikali ya pamoja itakapoundwa.

Suala la mipaka na idaidi ya majimbo limesalia tata, kati ya rais Kiir na mpinznai wake Riek Machar katika mchakato wa undwaji wa serikali hiyo.