Pata taarifa kuu
TANZANIA-MAGUFULI-UCHUMI-SIASA

Magufuli amteua waziri mpya wa mambo ya ndani

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, Dar es Salaam, Oktoba 30, 2015.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, Dar es Salaam, Oktoba 30, 2015. REUTERS/Sadi Said

Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua George Simbachawene kuwa waziri mpya wa mambo ya ndani baada ya kumfuta kazi mtangulizi wake Kangi Lugola.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imekuja baada ya kiongozi huyo kutofurahishwa na utendaji wa wizara hiyo chini ya aliyekuwa waziri wake Kangi Lugola.

Magufuli amesema licha ya kuwa rafiki wa karibu na Waziri huyo wa zanani,hawezi keundelea kuhudumu katika nafasi hiyo.

''Urafiki upo lakini katika suala la kazi siwezi kuruhusu na hivyo ndivyo nilivyo. Nakupenda sana lakini katika hili hapana, “ amesema rais Magufuli.

Kabla ya uteuzi huo George Simbachawene alikuwa Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia muungano na mazingira.

Rais Magufuli amemteua Musa Azan Zungu, mbunge wa Ilala kujaza nafasi iliyoachwa na Simbachawene.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.