SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Raia waendelea kusubiri Serikali ya umoja wa kitaifa Sudani Kusini

Kiongozi wa waasi Riek Machar (kushoto) na rais wa Sudani Kusini Salva Kiir wakisaini makubaliano ya kugawana madaraka huko Khartoum, Sudani, Agosti 5, 2018.
Kiongozi wa waasi Riek Machar (kushoto) na rais wa Sudani Kusini Salva Kiir wakisaini makubaliano ya kugawana madaraka huko Khartoum, Sudani, Agosti 5, 2018. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Kusini Riek Machar, amerejea jijini Khartoum, bila ya kuafikiana na rais Salva Kiir kuhusu masuala tata, kuelekea uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa tarehe 22 mwezi ujao.

Matangazo ya kibiashara

Machar alikuwa jijini Juba kwa kipindi cha wiki mbili, kufanya mazungumzo na rais Kiir na wadau wengine kuhusu masuala ya idadi ya majimbo na mipaka, na suala la usalama.

Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa, Machar anatarajiwa kurejea tena jijini Juba, kujaribu kuendelea na mazungumzo hayo.

Machar na Kiir wameshindwa kuunda serikali mara mbili licha ya kukubaliana, mwezi Mei na Novemba, mwaka 2019 baada ya mkataba wa amani mwaka 2018.