RWANDA-UGANDA-USHIRIKIANO

Kagame: Sintowaambia Wanyarwanda wasafiri kwenda Uganda

Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. SIA KAMBOU / AFP

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema amekuwa akiwaambia raia wa nchi yake kuacha kwenda nchini Uganda, kwa hofu ya kukamatwa au kuuawa.

Matangazo ya kibiashara

Kagame amewaambia Mabalozi wa mataifa mbalimbali jijini Kigali kuwa, amejitahidi kuambia uongozi wa nchi jirani ya uganda kuacha kuwakamata na kuwafunga raia wake, bila mafanikio na sasa njia pekee ya kuzuia hilo ni kuwaambia Wanyarwanda kutoenda katika nchi hiyo.

Mzozo wa Uganda na Rwanda ulianza kushuhudiwa mwaka uliopita, baada ya Rwanda kufunga mpaka wake wa Gatuna, huku Rwanda nayo ikilalamika kuwa Uganda inawatesa raia wake wanaoingia nchini humo.

Angola imekuwa ikijaribu kusuluhisha mzozo kati ya Kampala na Kigali, lakini inaonekana juhudi zinapigwa polepole.

Uganda hivi karibuni, iliwaachilia huru, raia tisa wa Rwanda ambao walikuwa wameshtakiwa kwa madai ya kutishia usalama wa nchi hiyo.