SUDANI-UN-USALAMA

Sudani Kusini: Umoja wa Mataifa washtumu pande zinazohasimiana kuwaua raia na njaa

Wakimbizi wa ndani, raia wa Sudani Kusini katika kambi ya Bentiu wakipokea chakula kilichotolewa na Umoja wa Mataifa.
Wakimbizi wa ndani, raia wa Sudani Kusini katika kambi ya Bentiu wakipokea chakula kilichotolewa na Umoja wa Mataifa. REUTERS/David Lewis

Umoja wa Mataifa umetoa ripoti mpya kuhusu Sudani Kusini, baada ya ripoti kadhaa au taarifa kama hizo ambazo hazijazaa matunda yoyote, huku raia wakiendelea kukumbwa na visa mbalimbali.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umeishtumu serikali ya Sudani Kusini na kundi la waasi linaloongowza na Riek Machar kushindwa kutafutia suluhu matatizo yanayoikabili nchi hiyo na hivyo kusababisha mamilioni ya raia kukabiliwa na njaa.

"Mamilioni ya raia wa Sudani Kusini amekataliwa kwa makusudi kupata huduma za msingi na wengi wanakabiliwa na njaa, wakati mapato ya kitaifa yamepitishwa mlango wa nyuma na wanasiasa wa nchi hiyo," inasema ripoti ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu kuhusu Sudani Kusini.

Ripoti hii yenye kurasa hamsini inaelezea udhalilishaji unaofanywa na pande zinazohasimiana kati ya mwezi Septemba 2018, tarehe ya ambapo mkataba wa mwisho ya amani ulitiliwa saini, na mwezi Desemba mwaka jana.