RWANDA-UGANDA-RUTABANA-HAKI

Uchunguzi: Benjamin Rutabana ashikiliwa na idara ya ujasusi ya Uganda

Benjamin Rutabana, mwanamuziki na mpinzani wa Rwanda.
Benjamin Rutabana, mwanamuziki na mpinzani wa Rwanda. DR

Uchunguzi uliofanywa na shirika la kutetea haki za binadamu la Marekani, International Relief and Human Rights Initiative (IRHRI), umehitimisha kwamba Benjamin Rutabana alikamatwa alipowasili nchini Uganda na idara ya ujasusi ya nchi hiyo (MCI), ambayo inamshikilia tangu wakati huo.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu la Marekani, IRHRI, limeamua kuwasilisha malalamiko yake mbele ya majaji.

Wengi wanahoji kuhusu ukweli wa habari hii na huenda inaleta faraja na matumaini kwa familia ya Benjamin Rutabana.

Benjamin Rutabana, Mwanamuziki na mpinzani wa Rwanda alitoweka tangu mwezi Septemba 2019 alipokuwa nchini Uganda na alijaribu kujiunga na kundi la waai wa Rwanda la RNC, lenye makao yake Kaskazini mashariki mwa DRC.

Uchunguzi uliofanywa na shirika hilo la haki za binadamu la Marekani, limewasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama ili mkosoaji huyo wa utawala wa Paul Kagame afikishwe majakamani.

Kufikia sasa, familia ya Ben Rutabana inajua kwamba ndugu yao alitoweka kufuatia malumbano ya ndani katika kundi la waasi wa Rwanda la RNC.

Benjamin Rutabana ni mmoja wa makada wakuu wa kundi la waasi la RNC, ambalo serikali ya Kigali inalichukulia kama kundi la kigaidi.

Wakati wa kutoweka kwake, Benjamin Rutabana alikuwa kwenye mpaka wa Uganda na DRC, ambapo alikuwa anakwenda kujiunga na wapiganaji wa kundi lake.

Wakati huo, alikuwa akivutana na kiongozi wa RNC, Kayumba Nyamwasa. Familia ya Rutabana ilimshtumu Kayumba Nyamwasa kuhusika na kitendo hicho, huku familia ya Nyamwasa ikinyooshea kidole cha lawama serikali ya Rwanda, ambayo ilikanusha.

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na shirika la haki za binadamu la Marekani, International relief and Human rights initiative, jaji wa mahakama ya Uganda aliitaka idara ya usalama kumfikisha Ben Rutabana mbele ya Mahakama Kuu ya haki jijini Kampala tarehe 19 Februari, jambo ambalo halikufanyika.

Jaribio lingine lilifanyika Alhamisi iliyopita. wakati huo viongozi wa idara zote za usalama waliwasili mahakamani na kusema kwa pamoja kwamba idara wanazoongoza hazimshikilii Ben Rutabana, isipokuwa tu idara ya ujasusi ya Uganda (MCI), inayoshtumiwa kumkamata mpinzani huyo wa Rwanda mwezi Septemba 2019 .

Jaji Esta Nambayo ameiagiza idara ya ujasusi kuripoti mbele ya Mahakama Kuu ya Kampala Alhamisi hii, Machi 5 asubuhi.