UGANDA-SISA-USALAMA

Makaazi ya Luteni Jenerali mstaafu Henry Tumukunde yazingirwa na Polisi

Maafisa wa usalama nchini Uganda wamezingira makaazi ya Luteni Jenerali mstaafu Henry Tumukunde katika Wilaya ya Rukungiri, hatua inayokuja baada ya kukamatwa wiki iliyopita kwa madai ya uhaini.

Rais Yoweri Museveni amekubali ombi kutoka kwa Wabunge wa Jimbo la Buganda kupeperusha bendera ya chama cha NRM katika uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2021.
Rais Yoweri Museveni amekubali ombi kutoka kwa Wabunge wa Jimbo la Buganda kupeperusha bendera ya chama cha NRM katika uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2021. .gov.ug jpg
Matangazo ya kibiashara

Tumukunde amejikuta mikononi mwa maafisa wa usalama baada ya wiki kadhaa kutangaza kuwa atawania urais kupambana na kiongozi wa sasa Yoweri Museveni, mwaka ujao.

Upinzani umeendelea kumnyooshea kidole cha lawama rais Yoweri Museveni kwa kuminya demokrasia nchini Uganda, hasa kwa kuwanyamanzisha wapinzani.

Rais Museveni, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 71, aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 1986, na tangu hapo ametajwa kama mmoja wa viongozi barani Afrika, waliojipendekeza kwa nchi za Magharibi kwa kupambana na ugaidi.

Wakosoaji wa Museveni wanasema kiongozi huyo mkongwe anafuata njia potofu ya viongozi wa Afrika wanaojaribu kukaa madarakani maisha yao yote, huku wakipuuza wito wa kuzingatia ukomo wa kuwapo madarakani.

Museveni aliyeongoza vita vya msituni na kumuingiza madarakani katika miaka ya 1980, amekuwa akihusishwa na juhudi za kuleta amani na kuinua uchumi wa Uganda, ingawa bado nchi hiyo inayotazamiwa kuwa mzalishaji mkuba wa mafuta ina changamoto kubwa ya miundombinu duni.

Wakosoaji wanampinga kwa kusema kuwa hakufanya jitihada za kutosha za kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na pia kwenye vita dhidi ya ufisadi. Pia anakosolewa kwa kushindwa kusogeza madaraka kwenye ngazi za chini katika juhudi zake za kuiendeleza Uganda.