RWANDA-USALAMA-SIASA

Rwanda yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 26 ya mauaji ya kimbari

Mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani yalitokea mwaka 1994 nchini Rwanda.
Mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani yalitokea mwaka 1994 nchini Rwanda. RFI/Stéphanie Aglietti

Rwanda imeanza kipindi cha maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 26 ya maua ji ya kimbari ambapo zaidi ya watu 800,000, wengi wakiwa kutoka kabila la Watutsi waliouawa kikatili mwaka 1994.

Matangazo ya kibiashara

Huu ni mwaka wa 26 na tofauti na miaka iliyopita, maadhimisho ya mwaka huu hayajafanyika kutokana na maambukizi ya Corona.

Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalianza siku moja baada ya ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana kudunguliwa mjini Kigali Aprili 6, mwaka 1994 na kumuua kiongozi huyo kutoka kabila la wengi la Wahutu pamoja na rais wa Burundi Cyprien Ntaryamira.

Watutsi walio wachache walishutumiwa kwa kuidungua ndege hiyo na hatimaye wapiganaji wenye msimamo mkali wa Kihutu wakaanzisha mauaji dhidi ya Watutsi, huku wakisaidiwa na jeshi, polisi pamoja na wanamgambo.

Imeelezwa kuwa katika miaka ya nyuma kumbukumbu hizo zilikuwa zikisababisha machungu na maumivu makali kwa baadhi ya watu, huku wengi wao wakiangua vilio, wakitetemeka, wakipiga kelele au hata kuzimia katikati ya mkesha huo wa kumbukumbu. Bado imekuwa vigumu kwa waathirika kadhaa kusamehe, kutokana na miili ya wapendwa wao kutojulikana ilipo na pia wauawaji wengi kuwa huru.