KENYA-CORONA-AFYA

Watu 114 wapona ugonjwa wa Covid-19 Kenya, idadi ya maambukizi yaongezeka

Wafanyakazi wa afya wa Kenya wakiwa wamevalia mavazi maalumu ya kujikinga na maambukizi ya Corona wakitafuta makazi ya mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa nchini Kenya kuwa na ugonjwa wa Covid-19, katika eneo la Rongai karibu na Nairobi, Kenya Machi 14, 202
Wafanyakazi wa afya wa Kenya wakiwa wamevalia mavazi maalumu ya kujikinga na maambukizi ya Corona wakitafuta makazi ya mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa nchini Kenya kuwa na ugonjwa wa Covid-19, katika eneo la Rongai karibu na Nairobi, Kenya Machi 14, 202 REUTERS/Baz Ratner

Kenya inasema wagonjwa waliopona virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 144 , lakini hadi sasa imeshuhudia vifo 17, huku watu zaidi ya Elfu 20 wakipimwa kufikia tarehe 30 mwezi Aprili mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, idadi ya maambukizi imeongezeka na kufikia 396 kufikia siku ya Alhamisi akiwemo mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Katika hatua nyingine, Maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika yamefikia zaidi ya 35,000 na vifo zaidi ya 1,500.

Tanzania sasa inakuwa na idadi kubwa ya wagonjwa kati ya nchi za Afrika Mashariki, wakati huu Shirika la afya duniania WHO likisema nchi hiyo ilichelewa kuchukua hatua za haraka kudhibiti kuenea kwa mamabukizi hayo kwa kasi.

Nchi ya Kenya inachukuwa nafasi ya pili kati ya nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa na wagonjwa wengi wa Corona baada ya Tanzania ambayo inaongoza kwa wagonjwa 396 wa Corona.

Hata hivyo serikali ya Kenya imepiga marufuku kuingia na kutoka katika kambi mbili kubwa za wakimbizi za Dadaab na Kakuma, katika jitihada za kusaidia kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.