TANZANIA-CORONA-AFYA

Rais Magufuli hakubaliani na tawimu zilizotolewa kuhusu Corona

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli Oktoba 2015.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli Oktoba 2015. REUTERS/Sadi Said

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amehoji ukweli kuhusu takwimu zilizotolewa na serikali kuhusu janga la Covid-19 na kuagiza uchunguzi ufanyike kwa maabara ya kitaifa ya matibabu.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake, Magufuli amesema, "hali sio mbaya kama vile wanavyodai walalamikaji.

Rais Magufuli amesema sampuli kadhaa ambazo hazikuwa za binadamu zilitumwa katika maabara ya taifa hilo ili kupima ubora na usahihi wa majibu ya mashine hizo katika vipimo vya ugonjwa huo.

''Sampuli hizo zilipewa majina ya binadamu na kupelekwa bila ya wataalamu wa maabara kujua kuwa si za bidanamu'', amebaini Magufuli.

"Sampuli ya oili ya gari ilipewa jina la Jabiri Hamza na haikukutwa na Corona. Sampuli ya Tunda la fenesi ilipewa jina la Sara Samuel majibu yake hayakukamilika, sampuli ya papai iliitwa Elizabeth na kukutwa na Corona. Sampuli ya ndege kwale pia ilikutwa na Corona pamoja na mbuzi pia, " ameongeza rais wa Tanzania.

Wakati huo huo upinzani umemshutumu rais huyo kwa kupuuzia hali inayojiri kwa sasa.

Tanzania imesalia moja ya nchi chache barani Afrika ambazo hazijachukua hatua za kali dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. Visa 480 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa rasmi nchini Tanzania, pamoja na watu 16 ambao wamefariki dunia. Idadi ambayo rais Magufuli amefutilia mbali.

"…Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii. Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa," alisema Magufuli.

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, kimemtuhumu rais Magufuli kupuuzia hali inayojiri nchini humo. Baada ya vifo vya wabunge watatu wanaoshukiwa kufariki dunia kutokana na Covid-19, siku ya Ijumaa chama hicho kiliwatolewa wito wajumbe wake kutoshiriki vikao vya bunge.

Chama cha Chadema kinasema, hatua madhubuti ni muhimu, lakini rais Magufuli hataki kusikia hivo. Sio tu kwamba biashara na sekta ya uchukuzi zinaendelea kufanya kazi kawaida, lakini Jumapili rais alisema kwamba ana mpango wa kuanzisha tena michuano ya Ligi ya kuu.