KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus Kenya: Baadhi ya raia wasusia kampeni ya vipimo

Baadhi ya Wakenya wanakataa kupimwa. Wana hofu kwamba watapatikana na virusi vya Corona na hivyo kuwa katika hatari ya kifo.
Baadhi ya Wakenya wanakataa kupimwa. Wana hofu kwamba watapatikana na virusi vya Corona na hivyo kuwa katika hatari ya kifo. REUTERS/Baz Ratner

Kenya imefanya zaidi ya vipimo 20,000 tangu kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya Corona kuripotiwa nchini humo Machi 13 mwaka huu. Serikali nchini humo ilikuwa inatarajia kuwapima maelfu ya watu, lakini ni mamia tu ndio wanaojitokeza.

Matangazo ya kibiashara

Kenya inatarajia kufikia vipimo 250,000 ifikapo mwezi Juni mwaka huu. Lakini hakuna uhakika kuwa lengo hilo litafikiwa sababu baadhi ya watu wana hofu ya kuwekwa karantini.

Baadhi ya Wakenya wanakataa kupimwa. Wana hofu kwamba watapatikana na virusi vya Corona na hivyo kuwa katika hatari ya kifo.

Mwishoni mwa mwezi Machi, mamlaka ilifungua karibu maeno hamsini, shule, hoteli, kumbi za vijana kwa kuwapokea watu wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Corona. Lakini, Wakenya ndio walitakiwa kulipa gharama za huduma, kutoka dola 20 hadi dola 100 kwa siku. Hali ambayo ilikuwa ngumu miongoni mwa raia hao, hasa wafanyikazi wanaolipwa kwa siku.