KENYA-CORONA-AFYA

Coronvirus: Maambukizi ya virusi vya Corona yapindukia 535 Kenya

Kenya inatarajia kufikia vipimo 250,000 ifikapo mwezi Juni mwaka huu. Lakini hakuna uhakika kuwa lengo hilo litafikiwa sababu baadhi ya watu wana hofu ya kuwekwa karantini.
Kenya inatarajia kufikia vipimo 250,000 ifikapo mwezi Juni mwaka huu. Lakini hakuna uhakika kuwa lengo hilo litafikiwa sababu baadhi ya watu wana hofu ya kuwekwa karantini. REUTERS/Baz Ratner

Waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa visa vya maambukizi vimefikia 535 baada ya visa vipya 45 ndani ya saa 24. Kufikia sasa Kenya ugonjwa wa Covid-19 umeua watu 24 na 173 wamepona.

Matangazo ya kibiashara

Visa hivi vipya vinakuja wakati siku ya Jumamosi serikali ilichukuwa hatua za kulegeza masharti ya raia kutotembea na kuruhusu migahawa kufunguliwa tena wakati wa mchana kuanzia saa 11 asubuhi na saa 10 jioni.

Watakaoingia kuhudumiwa watahitajika kufuata utaratibu uliopo wa kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa kama kawaida. Hatua ya kutokaribiana itaendelea kutekelezwa umbali wa mita 1 baina ya mtu mmoja hadi mwengine.

Hata kama wakazi wa jiji la Nairobi wameruhusiwa kutembea, na kufanya shughuli zao, amri ya kutotoka nje ilitangazwa siku ya Ijumaa Machi 27, 2020 kuanzia saa 1:00 usiku hadi saa11:00 asubuhi. Safari kati ya miji mikubwa pia ni imepigwa marufuku.

Kufikia sasa Kenya imefanya zaidi ya vipimo 20,000 tangu kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya Corona kuripotiwa nchini humo Machi 13 mwaka huu. Serikali nchini humo ilikuwa inatarajia kuwapima maelfu ya watu, lakini ni mamia tu ndio wanaojitokeza.

Kenya inatarajia kufikia vipimo 250,000 ifikapo mwezi Juni mwaka huu. Lakini hakuna uhakika kuwa lengo hilo litafikiwa sababu baadhi ya watu wana hofu ya kuwekwa karantini.