UGANDA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Shughuli za kawaida zaanza kurejea Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Capture d'écran al-Jazeera

Rais Yoweri Museveni amewataka wananchi wa Uganda na raia wa kigeni waishio nchini humo kuvaa barakoa na kusema uvaaji wa Barakoa ni jambo la lazima nchini humo kuanzia Jumanne wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Uganda imeungana na baadhi ya nchi zingine za Afrika kama vile Ghana, Afrika Kusini, Kenya Rwanda na Nigeria kwa kulegeza masharti ya raia kutotembea.

Katika hotuba yake Jumatatu usiku, Museveni amesema kuwa kuruhusu shughuli kuendelea kama awali inabidi kufanyike kwa umakini na mpangilio ili kuzuia virusi kusambaa kwa kasi.

Hatua hiyo imetangazwa wakati Waganda walikuwa na siku 35 hawatoki nyumbani kufuatia marufuku ya kutotoka nje ama 'lockdown' iliyowekwa na serikali.

Hata hivyo rais Museveni amesema marufuku ya awali bado inaendelea ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa mipaka ya nchi, kutoruhusu usafiri binafsi na wa umma, mikusanyiko ya watu na marufuku ya kutotoka nje usiku bado. Vizuizi hivyo bado vitatumika kwa kipindi kingine cha siku 14, ameongeza Museveni.

Jumatatu wiki hii Rwanda na Nigeria zilianza kulegeza masharti ya raia kutotembea kama sehemu ya mapambano dhidi ya Corona.

Kufikia sasa Uganda ina visa 97 vya maambukizi ya virusi vya Corona, baada ya visa vipya 8 kuthibitishwa ndani ya saa 24