WHO-TANZANIA-MAGUFULI-CORONA-AFYA

Shirika la Afya Dunia: Madai ya rais wa Magufuli hayana ukweli wowote

Katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa WHO barani Afrika Matshidiso Moeti amesema hawakubaliani na mtazamo wa Magufuli.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa WHO barani Afrika Matshidiso Moeti amesema hawakubaliani na mtazamo wa Magufuli. CC/Wikimedia/Jude Morel

Shirika la Afya Duniani WHO limefutlia mbali madai ya rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwamba vipimo vya virusi vya corona vina kasoro. Wakati huo huo kituo cha kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika kimekanusha madai hayo ya rais wa Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Jumapili iliyopita rais Magufuli alisema kwamba vipimo hivyo vina kasoro baada ya kuonyesha maambukizi ya virusi vya Corona katika majimaji ya tunda la papai na mbuzi.

Mara ya mwisho kwa eneo hilo kutangaza idadi mpya ya wagonjwa ilikuwa Jumatano iliopita ambapo wagonjwa 480 walithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Hatua hiyo imezua wasiwasi kuhusu jinsi taifa hilo linavyokabiliana na ugonjwa huo.

Hali hiyo inatokea wakati serikali ya nchi hiyo ikiwa inakosolewa juu ya namna inavyolishughulikia janga la Corona.

Kufikia sasa taarifa rasmi ni kuwa, nchi hiyo imethibitisha wagonjwa 480 na vifo 10, pamoja na watu 167 kupona.

Idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19 kote duniani imeongezeka na kufikia zaidi ya watu 263,000 huku watu milioni 3.7 wakiwa wameambukizwa.

Hayo yanajiri wakati nchi jirani ya Kenya imetangaza visa 607 vya maambukizi ya virusi vya Corona, baada ya visa vipya 25 kuthibitishwa nchini humo.