EAC-CORONA-AFYA-UCHUMI

Jumuiya ya Afrika Mashariki wakubaliana kushikamana katika vita dhidi ya Covid-19

Madereva wa malori wanajiandaa kufanya vipimo vya Corona kwenye eneo la mpakani la Namanga kati ya Kenya na Tanzania, huko Namanga, Kenya, Mei 12, 2020.
Madereva wa malori wanajiandaa kufanya vipimo vya Corona kwenye eneo la mpakani la Namanga kati ya Kenya na Tanzania, huko Namanga, Kenya, Mei 12, 2020. REUTERS/Thomas Mukoya

Viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana, kushirikiana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Corona na kubadilishana taarifa muhimu.

Matangazo ya kibiashara

Marais wa mataifa hayo sita, walikuatana kwa mfumo wa video siku ya Jumanne lakini rais wa Tanzania John Magufuli na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hawakuhudhuria kikao hicho.

Siku za hivi karibuni, kumekuwa na wasiwasi kuwa ongezeko la maambukizi ya corona, sasa linatokea katika maeneo ya mipakani na wanaopatikana na maambukizi hayo kwa wingi ni madereva wa malori.

Kumekuwa na madai kuwa Tanzania na Burundi, hazitoi ushirikiano wa kutosha ndani ya Jumuiya katika vita dhidi ya maambukizi hayo, madai ambayo nchi hizo zimeendelea kukanusha.

Hayo yanajiri wakati nchini Kenya, idadi ya maaambukizi ya virusi vya Corona imefikia 715, baada ya watu wengine 15 kuambukizwa kwa muda wa saa 24 zilizopita.

Mbali na ongezeko hilo, Wizara ya afya inasema idadi ya watu waliopona pia imeongezeka na sasa imefikia 259.