KENYA-CORONA-AFYA

Idadi ya wagonjwa wa Corona yapindukia 756 Kenya

Afisa wa manispaa akinyunyuzia dawa katika eneo la Kawangware jijini Nairobi mapema Mei 2020.
Afisa wa manispaa akinyunyuzia dawa katika eneo la Kawangware jijini Nairobi mapema Mei 2020. REUTERS/Baz Ratner

Watu wengine 21 wameambukizwa viruis vya Corona nchini Kenya na kufanya idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona kufikia 758. Kenya inaongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi katika mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na maambukizi hayo mapya, watu wengine wawili wamepoteza maisha na kufanya idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia 42, na watu 284 wamethibitishwa kupona ugonjwa huo.

Katibu katika Wiara ya afya nchini humo Mercy Mwangangi amesema mapambano zaidia sasa yamepelekwa mipakani baada ya madereva wengine wanane kutoka Tanzania kubaininika na virusi hivyo.

Katika kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona nchini Kenya, serikali imewaagiza madereva wote wa malori ya masafa marefu kufanyiwa vipimo vya lazima saa 48 kabla ya kuanza safari zao.

Hivi karibuni serikali ya Kenya ilichukuwa hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona, kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.

Hayo yanajiri wakati mwishoni mwa wiki iliypita, Wakenya waliokuwa wamekwama nchini India waliwasili nchini humo.