TANZANIA-UCHUMI

Serikali ya Tanzania yawatahadharisha wafanyabiashara wa bidhaa ya sukari

Vue de Dar es-Salaam plus grande ville de Tanzanie.
Vue de Dar es-Salaam plus grande ville de Tanzanie. Wikimedia/Chen Hualin

Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa sukari kwa wiki kadhaa sasa ambapo kiwango kidogo cha bidhaa hiyo kilichopo katika baadhi ya maduka, bei imepanda mara dufu, serikali imewatuhumu wafanyabiashara kwa kuficha sukari na kusababisha uhaba huo.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali hiyo, serikali imetoa kibali kwa wafanyabiashara nchini humo kuagiza toni 40,000 ili kuondokana na upungufu huo.

Katika maduka makubwa, sokoni na hata katika maduka ya kawaida kupata sukari imekuwa ni kuzungumkuti , Wananachi wametahadharishwa.

Serikali imetangaza bei kikomo kuwa isizidi Shilingi za Kitanzania 3,200 kwa kilo moja ya sukari, hivyo mikoa mingi kuuzwa kati ya 2,800 na 3,000, sawa na ongezeko la asilimia 23 kulingana na bei ya kawaida.

Hali hiyo imechangiwa na sababu mbalimbali, Mamlaka nchini Tanzania zinasema kila ifikapo mwezi machi viwanda husimamisha uzalishaji ili kufanya ukarabati, wakati kilimo cha miwa kikianza. Msimu huu hali ya kilimo cha zao hilo imekuwa tofauti kutokana na mvua nyingi na hivyo kuathiri ubora wa miwa na hivyo kuathiri uzalishaji kuanza mapema.

Serikali inawalaumu wafanyabiashara kwa kuficha sukari iliyokuwepo ili kusababisha uhaba na hivyo bei kupanda.

Serikali ya Tanzania inawataka wananchi kutoa taarifa ya wafanyabiashara wanaokiuka bei elekezi kulingana na mkoa waliopo.

Serikali ya Tanzania tayari imeruhusu uingizwaji wa sukari tani 40,000, sasa wananchi wanasubiri kuona ni lini adha hii itakwisha.