TANZANIA-CORONA=AFYA

Tanzania yatakiwa kutoa takwimu mpya za maambukizi ya Corona

Serikali ya Tanzania inasema kwa sasa kipaumbele chake kipo kwenye uchunguzi wa maabara kuu ya kupima virusi hivyo.
Serikali ya Tanzania inasema kwa sasa kipaumbele chake kipo kwenye uchunguzi wa maabara kuu ya kupima virusi hivyo. REUTERS/Sadi Said

Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC kinaitaka serikali ya Tanzania kutoa takwimu mpya za mwenendo wa maambukizi ya Corona nchini humo, ikiwa ni wiki mbili tangu nchi hiyo ilipotoa hali ya mamabukizi hayo.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa kituo ambacho kiko chini ya Umoja wa Afrika, Daktari John Nkengasong amesema utoaji wa takwimu za takwimu hizo ni kwa faida ya Tanzania.

Wizara ya afya nchini Tanzania hivi karibuni ilisema kuwa inaendelea kuyafanyia marekebisho maabara yake, kabla ya kuanza tena kutoa takwimu hizo, huku kwa upande mwingine wakosoaji wa serikali nchini humo wakiishtumu kwa kutosema kweli kuhusu mwenendo wa maambukizi hayo.

Mara ya mwisho kwa Tanzania Bara kutangaza takwimu mpya za corona ilikuwa wiki mbili zilizopita Aprili 29, huku Zanizbar ikitoa takwimu mpya kwa mara ya mwisho wiki moja iliyopita Mei 7.

Mpaka sasa, watu 509 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona nchini Tanzania, huku 183 wakipona na watu 21 kufariki dunia.

Serikali ya Tanzania inasema kwa sasa kipaumbele chake kipo kwenye uchunguzi wa maabara kuu ya kupima virusi hivyo.