RWANDA-UFARANSA-ICC-KABUGA-HAKI

Rwanda: Kinachomsubiri Félicien Kabuga, 'mfadhili' wa mauaji ya kimbari

Picha za baadhi ya wahanga wa mauaji ya kimbari waliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 zilizobandikwa kwenye ukuta wa jumba yanakohifadhiwa mabaki ya wahanga haokatika moja ya majumba ya ukumbusho Kigali.
Picha za baadhi ya wahanga wa mauaji ya kimbari waliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 zilizobandikwa kwenye ukuta wa jumba yanakohifadhiwa mabaki ya wahanga haokatika moja ya majumba ya ukumbusho Kigali. ©REUTERS/Baz Ratner

Félicien Kabuga, mfanyabiashara, anayeshtumiwa kufadhili mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliyotendeka mnamo mwaka 1994 nchini Rwanda atahukumiwa na Kitengo kinachohusika na kufunga faili za mwisho za mahakama za kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Félicien Kabuga, aliyekamatwa Mei 16 nchini Ufaransa, nyumbani kwake huko Asnières sur Seine katika vitongoji vya Paris, anatarajiwa kupelekwa Hague, nchini Uholanzi baada ya utaratibu wa mwisho kisheria nchini Ufaransa.

Félicien Kabuga, ambaye tayari amesikilizwa na ofisi ya mwendesha mashtaka ya Nanterre, anatarajiwa kusikilizwa tena na ofisi ya mwendesha mashtaka ya Paris mwanzoni mwa wiki hii. Baada ya utaratibu huo, kitengo cha mashitaka kitaundwa na kuamua kusafirishwa Hague.

Félicien Kabuga ahukumiwa na Kitengo maalumu, kitengo kilichoundwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2010 ili kuchukuwa nafasi ya mahakama zilizoundwa kwa minajili ya kushughulikia kesi za mauaji na uhalifu wa kivita vilivyotokea Yugoslavia ya zamani na Rwanda.

Kabuga anayetuhumiwa kuyafadhili makundi yaliyofanya mauaji hayo amekuwa anaukimbia mkono wa sheria kwa muda wa miaka 26.

Felicien Kabuga, alikuwa mtuhumiwa aliyewekwa kwenye mstari wa mbele. Kitita cha dola milioni tano kilitengwa kwa yeyote ambaye angetoa habari za kuwezesha kukamatwa kwake. Kwa muda wote huo alikuwa anatumia majina bandia.

Kwa mujibu wa taarifa ya mahakama ya Umoja wa Mataifa iIiyoanzishwa kwa ajili ya kuhumu kesi za uhalifu, IRMCT, Kabuga alihukumiwa mnamo mwaka mwaka 1997 kwa mokosa saba ya uhalifu ikiwa pamoja na ya mauaji ya halaiki, kuchochea mauaji na kushiriki katika mauaji.