RWANDA-UFARANSA-ICC-KABUGA-HAKI

Félicien Kabuga ataka ashtakiwe nchini Ufaransa

Waranti wa kukamatwa Félicien Kabuga ilichapishwa katika magazeti ya Kenya mwaka 2002.
Waranti wa kukamatwa Félicien Kabuga ilichapishwa katika magazeti ya Kenya mwaka 2002. REUTERS/George Mulala/File Photo

Félicien Kabuga, anayeshtumiwa kuwa "mfadhili mkuu" wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, amefikishwa kwa mara ya kwanza mbele ya jaji wa uchunguzi katika Mahakama Kuu ya Paris nchini Ufaransa Jumatano Mei 21.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu uwezekano wa kupelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, ili ahukumiwe kwa makosa ya "mauaji ya kimbari" na "uhalifu dhidi ya ubinadamu" yanayomkabili.

Kwa ombi la mawakili wake, kesi hiyo imeahirishwa Mei 27, wiki ijayo. Kabuga alisikilizwa kwa muda mfupi. Lakini ilionekana kuwa Félicien Kabuga anapinga kupelekwa mbele ya Mahakama hiyo ya kimataifa.

Akiulizwa kuhusu umri wake, Kabuga alisema kuwa ana umri wa miaka 87 na wala sio 84 kama inavyoandikwa kwenye waranti wa kukamatwa kwake.

Félicien Kabuga mwenye umri wa miaka 84, alikamatwa Jumamosi asubuhi huko Asnières-sur-Seine katika moja ya vitongoji wa mji wa Paris, nchini Ufaransa.