Serikali ya Sudani Kusini matatani, Mawaziri 10 waambukizwa corona
Imechapishwa:
Siku chache baada ya Makamu wa rais wa Sudani Kusini Riek Machar na mkewe kuthibitishwa kuwa virusi vya Corona, hatimaye mawaziri kumi wa sertikali ya nchi hiyo wameambukizwa virusi hivyo, kuwa mujibu wa msemaji wa serikali na pia Waziri wa Habari Michael Makuei.
Mawaziri wote 10 walikuwa ni wajumbe wa kamati ya juu ya serikali ya kupambana na Corona nchini humo.
Mawaziri wote 10 walioambukizwa virusi hivyo wamejitenga na wote wanaendelea vizuri kiafya, kulingana na taarifa ya serikali.
Sudani kusini ina wagonjwa wa Corona 481, na watu wanne wamepona na wengine wanne wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo hatari.
Virusi vya Corona vinaendelea kusababisha vifo na mdororo wa uchumi duniani kote, huku bara la Afrika likirekodi visa vya 96,829 vya maambukizi, na vifo 3,031 vinavyotokana na ugonjwa wa Covid-19 kulingana na kituo cha kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Corona cha Umoja wa Afrika, CDC
Kufiki sasa Covid-19 imeua watu 333,000 duniani kote, huku watu Milioni 5.11wakiwa wameambukizwa virusi hivyo.