Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi nchini Kenya yapindukia 1,214

Afisa wa afya katika manispaa ya jiji la Nairobi akinyunyuzia dawa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona katika eneo la Kawangware, Nairobi, Kenya, Mei 2, 2020.
Afisa wa afya katika manispaa ya jiji la Nairobi akinyunyuzia dawa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona katika eneo la Kawangware, Nairobi, Kenya, Mei 2, 2020. REUTERS/Baz Ratner
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Serikali ya Kenya inatoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi, kupimwa iwapo wana mamabukizi ya Corona. Katibu tawala wa wizara ya afya nchini Kenya Rashid Aman amesema kwamba idadi ya watu waliopimwa virusi hivyo kufikia sasa ni 59,260.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya nchini humo kuanzia wiki iliyopita, ilianza zoezi la kuwapima watu katika mitaa yao jijini Nairobi na mjini Mombasa.

Wito huu unekuja, wakati nchi hiyo ikiandikisha maambukizi mapya ya watu 22 na kufikisha idadi ya maambukizi kufikia 1,214 baada ya wagonjwa wapya 22 kuthibitishwa siku ya Jumapili. Wagonjwa 383 wamepona ugonjwa wa Covid-19, wakati watu 51wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Katika mkutano na waandishi wa habari, katibu tawala wa wizara ya afya nchini Kenya Rashid Aman amesema kwamba wagonjwa hao ni kati ya umri wa miaka 24 hadi 73 ,huku wanaume wakiwa 17 na wanawake wakiwa watano.

Rashid Aman amewataka Wakenya kuendelea kufuata maagizo ya serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.