Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Kenya yarekodi visa vipya 72 ndani ya kipindi cha saa 24

Moja ya mita ya maeneo ya Kibera jijini Nairobi, Kenya, Mei 22, 2020, ambapo watu wametakiwa kuvaa Barakoa katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.
Moja ya mita ya maeneo ya Kibera jijini Nairobi, Kenya, Mei 22, 2020, ambapo watu wametakiwa kuvaa Barakoa katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona. REUTERS/Baz Ratner

Watu wengine 72 wamebainika kuambukizwa virusi vya corona nchini Kenya na kufiisha idadi ya watu walioambukizwa kufikia 1,286. Wagonjwa 402 wameponaugonjwa huo ambao umeua watu 52.

Matangazo ya kibiashara

Idadi kubwa ya maambukizi hayo yameripotiwa katika jiji kuu la Nairobi.

Wakati ongezeko hili likishuhidiwa, serikali nchini humo inafikiria kurejesha shughuli za kawaida nchini humo hivi karibuni, wakati huu watalaam wa afya wakisema itabidi watu nchini humo waanze kuzoea kuishi na virusi hivyo.

Hivi karibuni serikali ya Kenya ilitoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi, kupimwa iwapo wana mamabukizi ya Corona. Katibu tawala wa wizara ya afya nchini Kenya Rashid Aman alisema kwamba idadi ya watu waliopimwa virusi hivyo kufikia sasa ni 59,260.

Wizara ya afya nchini humo kuanzia wiki iliyopita, ilianza zoezi la kuwapima watu katika mitaa yao jijini Nairobi na mjini Mombasa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.