Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Covid-19 yaendelea kuiathiri Kenya, maambukizi zaidi yathibitishwa

Madereva wa malori wanajiandaa kufanya vipimo vya Corona kwenye mpaka wa Namanga kati ya Kenya na Tanzania, huko Namanga, Kenya, Mei 12, 2020.
Madereva wa malori wanajiandaa kufanya vipimo vya Corona kwenye mpaka wa Namanga kati ya Kenya na Tanzania, huko Namanga, Kenya, Mei 12, 2020. Filbert RWEYEMAMU / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Wizara ya afya nchini Kenya, inasema idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini humo sasa imefikia 1,348, baada ya watu wengine 62 kuambukizwa kwa muda wa saa 24 zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa Kenya imerekodi vifo vya watu 52 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19, huku wagonjwa 405 wakithibitishwa kupona.

Wakati hayo yakijiri, biashara katika eneo la mpaka wa Lunga-Lunga kati ya nchi hiyo na Tanzania imeonekana kuyumba kutokana na janga hilo la Covid-19.

Magari yakiegesha kwenye eneo la mpaka la Lunga-Lunga kati ya Kenya na Tanzania, Mei 19, 2020.
Magari yakiegesha kwenye eneo la mpaka la Lunga-Lunga kati ya Kenya na Tanzania, Mei 19, 2020. Joseph Jira/RFI

Wakati ongezeko hili likishuhidiwa, serikali nchini humo inafikiria kurejesha shughuli za kawaida nchini humo hivi karibuni, wakati huu watalaam wa afya wakisema itabidi watu nchini humo waanze kuzoea kuishi na virusi hivyo.

Hivi karibuni serikali ya Kenya ilitoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi, kupimwa iwapo wana maabukizi ya Corona.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.