Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda: Félicien Kabuga kuhukumiwa Arusha, Tanzania
Imechapishwa:
Mahakama ya Rufaa ya Paris tangu Jumatano wiki hii inachunguza waranti wa kimataifa wa kukamatwa uliyotolewa dhidi ya mfadhili wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na mmoja wa wanzilishi wa redio Mille Collines iliyochochea mauaji nchini humo.
Mahakama ya Rufaa ya Paris inatarajia kutoa uamuzi wake kuhusu kupelekwa kwa Kabuga Felicien mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai mjini Hague, au mbele ya mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi ya mauaji ya Rwanda.
Wadadisi wanasema Kabuga Felicien huenda akahukumiwa jijini Arusha, nchini Tanzania.
Ombi la mwendesha mashtaka kwenye mahkama iliyochukuwa nafasi ya mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji nchini Rwanda, ambaye alitaka kumuona mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC huko Hague nchini Uholanzi, limekataliwa kwa sababu ya janga la Covid-19.
Wakati utaratibu wa Mahakama za Kimataifa ya Makosa ya Jinai ina vitengo viwili: moja huko Hague, na kingine jijini Arusha, nchini Tanzania, na kila upande unashughulikia kesi zake maalum. Kitengo cha kwanza, tawi la Ulaya, kina jukumu la kushughulikia kesi zilizosalia ambazo zingelipaswa kushughulikiwa na Mahakama ya Makosa ya Jinai kwa Yugoslavia. Kitengo cha pili, ni tawi la Afrika, ambacho kinashughulikia kesi za mauaji ya kimbari zilizosalia ambazo zilikuwa zikishughulikiwana Mahakama ya zamani ya Makosa ya Jinai ya Rwanda, ICTR.
Kumtuma Félicien Kabuga, hata kwa kipindi kifupi nchini Uholanzi, italazimika kurekebisha waranti wake wa kukamatwa.
Katika ombi lake, mwendesha mashitaka, Serge Brammertz, amebaini kwamba anahofia kwa sababu ya janga la Covid-19 na kufungwa kwa mipaka, Ufaransa itajikuta katika hali tata ikiwa Mahakama ya Rufaa ya Paris itathibitisha Félicien Kabuga kupelekwa nchini Tanzania.
Hiyo ni hofu tu, mmoja wa majai kwenye mahakama hiyo amesema. Amekumbusha kwamba kihistoria kuna muda wa "miezi mitatu hadi nane" kati ya kukamatwa nchini Ufaransa kwa mtuhumiwa na kumpeleka ICTR.
Ikiwa Mahakama ya Rufaa itatoa uamuzi wake wiki ijayo, upande wa utetezi unaweza kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi, hali ambayo iitaongeza muda wa utaratibu wa kisheria kwa wiki kadhaa.
Pia suala la mipaka linaweza kujadiliwa kwa kina. Na kama haitawezekana, kuna haja ya kutatmini tena suala hilo kwa muda muafaka ikiwa kumtuma mshtumiwa jijini Arusha haitawezekana.