Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kenya yaongoza kwa visa vya maambukizi Afrika Mashariki

Ugonjwa wa Covid-19 unaiathiri Kenya katika sekta mbalimbali.
Ugonjwa wa Covid-19 unaiathiri Kenya katika sekta mbalimbali. REUTERS/Thomas Mukoya

Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vimepindukia1,745 nchini Kenya baada ya watu 147 kuthibitishwa kupata maambukizi leo Ijumaa. Idadi ya vifo imefikia 62 baada ya vifo vipya 3 kuthibitishwa.

Matangazo ya kibiashara

Katibu wa Wizara ya Afya ya Kenya Dkt. Mercy Mwangangi, amesema idadi ya waliopona imefika 438 baada ya wagonjwa wengine 17 kuruhusiwa kuondoka hospitali katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Hayo uanajiri wakati visa vya maambukizi duniani kote imefikia Milioni 5.8. Wagonjwa Milioni 2;4 wamepona ugonjwa wa Covid-19, ambao umesababisha vifo vya watu 360,000, baada ya vifo 4,239 kuthibitishwa.

Kenya kwa sasa inaongoza kwa idadi kubwa ya visa vya maambukizi katika mataifa ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wakati ongezeko hili likishuhidiwa, serikali nchini humo inafikiria kurejesha shughuli za kawaida nchini humo hivi karibuni, wakati huu watalaam wa afya wakisema itabidi watu nchini humo waanze kuzoea kuishi na virusi hivyo.

Hivi karibuni serikali ya Kenya ilitoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi, kupimwa iwapo wana maabukizi ya Corona.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.