Pata taarifa kuu
UGANDA-CORONA-AFYA

Idadi ya maambukizi yapindukia 317 nchini Uganda

Uganda ilifanya maelfu ya vipimo kwa madereva wa malori, 51 kati yao, hususan Wakenya na Watanzania, walikutwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.
Uganda ilifanya maelfu ya vipimo kwa madereva wa malori, 51 kati yao, hususan Wakenya na Watanzania, walikutwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19. (c) Epicentre
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Uganda, imeongezeka na kufikia 317 baada ya watu wengine 36 kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Afya wa Uganda Ruth Aceng amesema visa hivyo vipya, vimeripotiwa miongoni mwa madereva wa malori waliongia nchini humo hivi karibuni na watu waliotangamana nao.

Hivi karibuni rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.

Rais Yoweri Museveni alibaini kwamba madereva hao ni chanzo cha wasiwasi kwa Uganda na ukanda mzima.

Uganda ilifanya maelfu ya vipimo kwa madereva wa malori, 51 kati yao, hususan Wakenya na Watanzania, walikutwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Hivi karibuni malori zaidi ya 300 yalikwama katika mpaka wa Namanga unaoziunganisha nchi za Kenya na Tanzania. Kundi la madereva wa magari makubwa ya kubeba mizigo linatajwa kusambaza virusi vya Corona kwa kiwango cha juu zaidi katika nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.