RWANDA-UFARANSA-ICC-KABUGA-HAKI

Hatma ya Félicien Kabuga kujulikana Jumatano hii

Félicien Kabuga, anayeshtumiwa kuwa mfadhili wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, hapa akioneshwa kwa katuni akiwa mahakamani Mei 20, 2020.
Félicien Kabuga, anayeshtumiwa kuwa mfadhili wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, hapa akioneshwa kwa katuni akiwa mahakamani Mei 20, 2020. Benoit PEYRUCQ / AFP

Félicien Kabuga, mfadhili wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani na mmoja wa wanzilishi wa redio Mille Collines iliyochochea mauaji nchini humo, anasubiri kujua hatma yake baada ya uamuzi wa mahakama ya Rufaa Jumatano wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Paris itaamua iwapo itamkabidhi Félicien Kabuga katika Mahakama maalum ya Kimataifa ambayo ilichukua nafasi ya ile iliyokuwa inashughulikia kesi za Kimbari nchini Rwanda iliyokuwa mjini Arusha nchini Tanzania.

Uamuzi wa majaji pia utajikita kuhusu uhalali wa waranti ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama Maalum ya Kimataifa ya IRMCT, mahakama ambayo ina majukumu ya kukamilisha kazi ya mahakama iliyokuwa inashughulikia kesi za Kimbari nchini Rwanda iliyokuwa mjini Arusha nchini Tanzania. Ikiwa waranti hiyo itachukuliwa kuwa ni halali, Félicien Kabuga atapata fursa ya kukata rufaa katika kitengo cha mahakama kuu, ambacho kitakuwa na miezi miwili ya kutoa uamuzi.

Kesi yake kesi yake huenda ikashughulikiwa huko Hague au jijini Arusha, nchini Tanzania.

Hata hivyo Félicien Kabuga anataka ashtakiwe nchini Ufaransa.

Hivi karibuni Mahakama ya Rufaa ya jijini Paris nchini Ufaransa ilitupilia mbali ombi la kuachiliwa kwa dhamana kwa Félicien Kabuga.

Kabuga amekuwa anaukimbia mkono wa sheria kwa muda wa miaka 26.

Félicien Kabuga, alikuwa mtuhumiwa aliyewekwa kwenye mstari wa mbele. Kitita cha dola milioni tano kilitengwa kwa yeyote ambaye angetoa habari za kuwezesha kukamatwa kwake. Kwa muda wote huo alikuwa anatumia majina bandia.

Kwa mujibu wa taarifa ya mahakama ya Umoja wa Mataifa iIiyoanzishwa kwa ajili ya kuhumu kesi za uhalifu, IRMCT, Kabuga alihukumiwa mnamo mwaka mwaka 1997 kwa mokosa saba ya uhalifu ikiwa pamoja na ya mauaji ya halaiki, kuchochea mauaji na kushiriki katika mauaji.

Félicien Kabuga mwenye umri wa miaka 84, alikamatwa Jumamosi asubuhi Mei 16 nchini Ufaransa, nyumbani kwake huko Asnières sur Seine katika vitongoji vya Paris, nchini Ufaransa.

Kabuga anashtmiwa makosa saba, ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na kufadhili makundi yaliyofanya mauaji ya kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda, ambapo watu zaidi ya 800,000 (Watutsi na Wahutu wa msimamo wa Wastani) waliuawa na wanamgambo wa Iterahamwe kutoka chama tawala wakati huo cha MRND cha hayati rais Juvenal Habyarimana.