Pata taarifa kuu
TANZANIA-ACT-SIASA-USALAMA

Kiongozi na mkosoaji wa utawala wa Magufuli akamatwa Lindi

Zitto Mwami Ruyagwa Kabwe (katikati), mmoja wa viongozi wa upinzai nchini Tanzania, alikamatwa huko Lindi, Kusini mwa nchi, 23/06/2020.
Zitto Mwami Ruyagwa Kabwe (katikati), mmoja wa viongozi wa upinzai nchini Tanzania, alikamatwa huko Lindi, Kusini mwa nchi, 23/06/2020. ACT Wazalendo/twitter.com
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo nchini Tanzania Zitto Mwami Ruyagwa Kabwe pamoja na wanachama wengine 8 wamekamatwa kwa kosa la kuandaa mkutano ambao haukuhalishwa mkoani Lindi, Kusini mwa Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha ACT Wazalendo kimethibitisha kukamatwa kwa kiongozi wake, kikisema ni mojawapo ya njama ya serikali kukandamiza upinzani kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Wakati huo huo, Serikali nchini humo imefuta leseni ya gazeti la Tanzania Daima linalohusishwa na upinzani nchini humo, kwa madai ya kukiuka sheria za uandishi na kuchapisha habari za uongo.

Kulingana na Sheria ya hudumaza habari, wachapishaji wa gazeti hilo wanayo fursa ya kuomba tena leseni kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari ili kuruhusiwa kurejea kuchapisha na kusambaza watakapoona wamejitafakari na kuwa tayari kufuata taratibu.

Wakati huo huo serikali ya Tanzania imeapa kuchukua hatua kali wakati wowote kwa watakaokiuka taratibu za kisheria na misingi ya taaluma muhimu ya habari.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.