BURUNDI-HRW-CORONA-AFYA

Corona: Burundi yanyooshewa kidole kwa kutishia maisha ya wahudmu wa afya

Timu ya wafanyakazi wa afya kutoka moja ya hospitali mjini Bujumbura, Burundi, Aprili 27, 2020.
Timu ya wafanyakazi wa afya kutoka moja ya hospitali mjini Bujumbura, Burundi, Aprili 27, 2020. Tchandrou Nitanga / AFP

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch, limeishtumu Serikali ya Burundi kwa kutishia maisha ya wahudmu wa afya wanaojaribu kutoa taarifa za kweli kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Human Rights watch inasema katika wiki za hivi karibuni, imewahoji wataalamu kadhaa na wahudumu wengine wa afya ambao wamethibitisha kuwa mamlaka nchini Burundi zimekuwa zikiwazuia wahudumu wa afya wanaojaribu kutoa takwimu za kweli za maambukizi ya virusi vya Corona kwenye taifa hilo ndogo la afrika ya kati.

Shirika hilo sasa linatoa wito kwa Rais mpya Evariste Ndayishimiye kuhakikisha raia wa nchi hiyo wanapata taarifa kamili kuhusu Covid-19, lakini pia na namna wanavyoweza kujikinga.

Aidha, Human Right Watch imesema Burundi imethibitisha visa zaidi ya 140 na kifo kimoja, na kwamba waliohojiwa na shirika hilo walionyesha wasiwasi juu ya kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa.

Serikali ya Gitega iliwafukuza maafisa watatu wa shirika la Afya Duniani, WHO, nchini humo mwezi Mei, huku maafisa wa serikali wakisema nchi hiyo inamtegemea Mwenyezi-Mungu katika vita dhidi ya virusi vya Corona.